From Wikipedia, the free encyclopedia
Filipo mwinjilisti ni Myahudi wa karne ya 1 anayejulikana hasa kutokana na Matendo ya Mitume.
Anaheshimiwa na madhehebu mbalimbali ya Ukristo kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa na Kanisa Katoliki na Anglikana tarehe 11 Oktoba[1][2], kumbe katika Makanisa ya Kiorthodoksi ni tarehe 6 Juni.
Alikuwa mmojawapo kati ya wanaume saba wa lugha ya Kigiriki katika Kanisa mama la Yerusalemu waliochaguliwa kushughulikia mafukara kwa niaba ya Mitume wa Yesu (Mdo 6).
Baadaye alijitokeza kama mhubiri na mtendamiujiza huko Samaria, alipoongoa na kubatiza wengi kati ya wakazi, bila kujali uadui wa jadi kati yao na Wayahudi (Mdo 8).
Baadaye aliongozwa na Mungu kuongozana na towashi muhimu wa Ethiopia akambatiza karibu na Gaza (Mdo 8).
Baadaye tena alikuwa akiishi Kaisarea Maritima, pamoja na mabinti wake wanne ambao walikuwa mabikira na manabii, Mtume Paulo alipopitia huko mwaka 58 akielekea Yerusalemu (Mdo 21)[3].
Mapema alianza kuchanganywa na Mtume Filipo, pia kwa sababu ya utume mkubwa alioufanya.[4]
Mapokeo ya baadaye yanasimulia kwamba alikuwa askofu wa Trale katika Uturuki wa leo.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.