Samaria
From Wikipedia, the free encyclopedia
Samaria (kwa Kiebrania שומרון, Shomron; kwa Kiarabu السامرة, as-Sāmirah), ni eneo la milimamilima katikati ya nchi inayoitwa Israeli au Palestina. Jina "Samaria" linatokana na lile la mji mkuu wa Ufalme wa Israeli.[1]


Kadiri ya 1Fal 16:24, jina la mji huo lilitokana na lile la Shemer, aliyemuuzia mfalme Omri eneo kwa ajili ya kuuanzisha kama makao makuu (884 KK hivi) badala ya Tirza.
Historia
Kadiri ya Biblia, Waisraeli waliteka eneo hilo la Kanaani na kulikabidhi kwa kabila la Yosefu.
Eneo lilitekwa na Waashuru mwaka 722 KK hivi, nao wakahamisha wakazi wake wengi hadi Mesopotamia. Badala yao waliletwa wengine kutoka huko. Ndiyo sababu wakazi wa eneo hilo wakaja kuwa wa mchanganyiko wakapewa jina jipya: "Wasamaria".
Baadaye lilitawaliwa na mataifa mbalimbali, kama vile Babuloni, Uajemi, Ugiriki wa kale, Dola la Roma, Bizanti, Waarabu, Wazungu wa vita vya msalaba, Waturuki na hatimaye Waingereza.[2]
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.