From Wikipedia, the free encyclopedia
Kasai Mashariki (Kasai-Oriental kwa Kifaransa) ni moja ya mikoa 11 ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Inapakana na mikoa ya Kasai Magharibi upande wa magharibi, Équateur upande wa kaskazini, Orientale upande wa kaskazini mashariki, Maniema upande wa mashariki na Katanga upande wa kusini. Kasai-Oriental ni kati ya maeneo duniani penye almasi nyingi. Makao makuu ya mkoa ni Mbuji-Mayi.
auto
Mkoa wa Kasai Mashariki | |
Nchi | Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo |
---|---|
Makao makuu | Mbuji-Mayi |
Serikali | |
- Gavana | Dominique Nkangu Kabengela |
Idadi ya wakazi (2005 est.) | |
- Wakazi kwa ujumla | 7,100,000 |
National language | Tshiluba |
Tovuti: kasaiest.cd |
Jina la mkoa latokana na mto Kasai.
Kasai-Oriental inakaliwa hasa na Waluba. Kabla ya ukoloni sehemu kubwa za mkoa zilkuwa chini ya milki ya Luba.
Wakati wa uhuru wa Kongo wanasiasa wa sehemu hii walijaribu kuanzisha dola la kujitegema ya Kasai kusini lakini jeshi la serikali kuu ilivamia eneo lake. Baada ya vita ya miezi minne iliyokuwa na wahanga maelfu eneo lilirudishwa Kongo na kugawiwa.
Eneo la mji wa Mbuji-Mayi linazalisha asilimia 10 ya almasi zote zinazotolewa duniani. Uchimbaji unasimamiwa na kampuni ya Société Minière de Bakwanga. Wananchi wengine wanajaribu kuchimba almasi kibinafsi. Kwa jumla wakazi wa mkoa hawafaidiki na utajiri huu.
Kifaransa ni lugha rasmi. Tshiluba ni lugha inayotumiwa na wakazi wengi ambacho ni moja ya lugha za kitaifa za Kongo.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.