Mkoa wa Équateur

From Wikipedia, the free encyclopedia

Mkoa wa Équateur
Remove ads

Mkoa wa Équateur (kwa Kiswahili: Mkoa wa Ikweta) ni mmojawapo kati ya mikoa 26 ya kujitawala ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Ukweli wa haraka Nchi, Wilaya ...

Idadi ya wakazi wake ni takriban 1,626,606.

Mji mkuu ni Mbandaka.

Mkoa huu ulianzishwa kutokana na ugawaji mpya wa mikoa kadiri ya katiba ya Kongo ya mwaka 2005. Kabla yake ilikuwa sehemu ya jimbo la Equateur pamoja na mikoa ya sasa ya Ubangi-Kaskazini, Mongala, Ubangi-Kusini na Tshuapa. Kabla ya kuingizwa katika jimbo la Equateur, wakati wa rais Mobutu Sese Seko, uliwahi kuwa mkoa wa pekee kati ya 1962-1966 kwa jina la Cuvette-Centrale.

Eneo la mkoa huu liko kaskazini-magharibi mwa nchi, kando ya mto Kongo. Upande wa magharibi unapakana na nchi ya Kongo-Brazzaville.

Sehemu kubwa ya Hifadhi ya Taifa ya Lomako Yokokala iko ndani ya mkoa huu. Hifadhi hii inajulikana hasa kwa sababu ndiko mahali pekee duniani wanapoishi nyani kubwa wa Bonobo wanaohesabiwa kati ya hominidi.

Remove ads

Wilaya

Mkoa umegawanywa katika mji wa Mbandaka na wilaya 7:

Picha

Viungo vya nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Makala hii kuhusu maeneo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mkoa wa Équateur kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads