Mji Mkongwe (kwa Kiingereza: Stone Town) ndio sehemu ya kale ya Jiji la Zanzibar, mji mkubwa wa kisiwa cha Unguja na mji mkuu wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.

Kama kitovu cha historia yake kilichoathiriwa na utamaduni wa Waarabu, wa Waajemi, wa Wahindi na wa Wazungu, Mji Mkongwe umeandikishwa katika orodha ya UNESCO ya "Urithi wa Dunia" (World Heritage).

Nyumba za Mji Mkongwe zilijengwa tangu mwaka 1830, wakati Sultani Sayyid Said alipohamisha mji mkuu wake kutoka Omani kuja Unguja.

Kati ya majengo maarufu ni Beit al Ajaib (Jumba la Maajabu lililobomoka tarehe 24 Desemba 2020[1]), Jumba la Sultani, Ngome Kongwe, Kanisa Kuu la Anglikana lililojengwa mahali pa soko la watumwa na hasa nyumba nyingi za kihistoria za ghorofa zilizojengwa na familia za tabaka la matajiri Waarabu zenye milango yenye mapambo mazuri.

Mji Mkongwe unapokea watalii wengi kila mwaka.

Mji wa kisasa umekua sana ng'ambo ya Mji Mkongwe.

Picha


Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Wikiwand in your browser!

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.

Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.