Mkoa wa Pwani (Kenya)
From Wikipedia, the free encyclopedia
Mkoa wa Pwani ni kati ya mikoa nane ya Kenya ukipakana na Bahari Hindi, Tanzania na mikoa ya Kenya ya Bonde la Ufa , Mashariki na Kaskazini-Mashariki.
Makao makuu ya mkoa yapo Mombasa.
Mkoani kuna wilaya zifuatazo (makao makuu katika mabano):
- Wilaya ya Lamu (Lamu)
- Wilaya ya Mto Tana (Hola)
- Wilaya ya Malindi (Malindi)
- Wilaya ya Kilifi (Kilifi)
- Wilaya ya Mombasa (Mombasa)
- Wilaya ya Kilindini (Mombasa)
- Wilaya ya Kwale (Kwale)
- Wilaya ya Kaloleni (Kaloleni)
- Wilaya ya Kinango (Kinango)
- Wilaya ya Taita-Taveta (Voi)
Mombasa ndipo ilipo bandari kuu ya Kenya. Kuna maeneo muhimu ya utalii kama Malindi na sehemu za pwani kusini (Diani)na kaskazini (Kikambala) ya Mombasa. Eneo la Voi katika mkoa wa Pwani ni maarufu kwa kulima makonge.