Mtumishi wa Mungu ni jina la heshima linalotumika katika Biblia na katika Ukristo kwa mtu anayesadikiwa kumtumikia Mungu kwa namna ya pekee.

Katika Biblia

Katika Biblia ya Kiebrania ni la juu kuliko "nabii", kwa sababu jina hilo lilikuwa na maana mbalimbali, hata mbaya, kwa mfano "kichaa" au "nabii wa uongo".

Katika Ukristo

Siku hizi linatumiwa na Wakristo wa madhehebu mbalimbali kwa maana tofauti.

Katika Kanisa Katoliki

Katika Kanisa Katoliki linatumika hasa[1] kwa waumini wafu ambao maisha yao yameanza kuchunguzwa ili kuona kama hatimaye wataweza kutangazwa watakatifu.[2][3]

Jina Mtumishi wa Mungu halimaanishi kuwa kweli mhusika alimtumikia Mungu kiaminifu hadi kifo chake, bali kwamba watu wengiwengi wanaona hivyo, hata askofu wa jimbo alifungua kesi ya kumtangaza mtakatifu.

Baada ya hatua hiyo kukamilika kwa Papa kuthibitisha ushujaa wa maadili yake yote, au kifodini chake, mtumishi huyo ataanza kuitwa Mstahili heshima.

Kisha kuthibitisha kwamba muujiza wowote umetokea kwa maombezi yake, Papa atamtangaza mwenye heri.

Baada ya muujiza mwingine atamalizia kwa kumtangaza mtakatifu.[4][5]

Kesi hizo katika hatua zote zinasimamiwa na idara maalumu yenye makao makuu huko Vatikani.

Tofauti na hilo ni jina Servus Servorum Dei (Mtumishi wa mtumishi wa Mungu), ambalo kuanzia Papa Gregori I linatumiwa na Mapapa kujitambulisha.

Tanbihi

Wikiwand in your browser!

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.

Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.