2001 (albamu)

From Wikipedia, the free encyclopedia

2001 (albamu)
Remove ads

2001 ni jina la albamu ya pili ya msanii na mtayarishaji wa muziki wa hip hop kutoka nchini Marekani - Dr. Dre. Albamu ilitolewa mnamo tar. 16 Novemba, 1999, kupitia studio za Interscope Records. Hili ni toleo la pili baada ya albamu ya kwanza ya Dr. Dre The Chronic (1992).

Ukweli wa haraka Studio album ya Dr. Dre, Imetolewa ...

Kimsingi ilitayarishwa na Dr. Dre na Mel-Man, na Lord Finesse, na kushirikisha michango kadha wa kadha kutoka kwa marapa wengine kama vile Hittman, Snoop Dogg, Kurupt, Xzibit, Nate Dogg, na Eminem. 2001 inadhihirisha upanuzi katika kuandaa midundo ya G-funk ambayo ina maudhui ya gangsta rap au rap ya kihuni au kisela - kukiwa na utata kama vile vurugu, uimbaji ovyo-ovyo, matumzi ya madawa ya kulevya, masela wa mtaa, na uhalifu.

Albamu iliingia moja kwa moja hadi nafasi ya pili kwenye chati za Billboard 200 huko nchini Marekani, na kuuza nakala 516,000 katika wiki yake ya kwanza. Ina vibao vyake vikali vitatu vilivyopelekea albamu kupata kupewa ngazi ya platinamu na RIAA kwa kufanya mauzo yake ya nakala milioni sita nchini Marekani pekee.

Licha ya hali yake ya kupondwa dhidi ya maudhui na mashairi yake ya kihuni/kisela sana, 2001 imepokea tahakiki mwanana kutoka kwa wataalamu wa kutathmini muziki. Albamu ilisifiwa na watunzi wa nyimbo wa kudumisha mtindo wa West Coast hip hop baada ya kimya cha miaka mingi, wakati anaonesha hilo Dr. Dre anaweza kubaki kuwa maarufu hata kwa wasikilizaji wa kizazi kipya.

Remove ads

Mapokeo ya kitahakiki

Ukweli wa haraka Makadirio ya kitaalamu, Tahakiki za ushindi ...

Orodha ya nyimbo

  • Nyimbo zote zimetayarishwa na Dr. Dre na Mel-Man, kasoro "The Message" imetayarishwa na Lord Finesse.
Maelezo zaidi No., Jina ...
Remove ads

Chati zake

Maelezo zaidi Mwaka, Chati ...

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya Nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads