50 Cent

From Wikipedia, the free encyclopedia

50 Cent
Remove ads

Curtis James Jackson III (amezaliwa tar. 6 Juni 1975) ni mwanamuziki wa rap-hip hop, mwigizaji na mtayarishaji kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama 50 Cent.

Ukweli wa haraka Maelezo ya awali, Jina la kuzaliwa ...

Ameanza kupata umaarufu zaidi baada ya kutoa albamu yake ya "Get Rich or Die Tryin" na 'The Massacre'. 50 Cent amepata Plantinam nyingi na mafanikio makubwa katika albamu zake mbili, aliuza nakala zaidi ya Mil. 21 kwa hesabu ya dunia nzima.

Remove ads

Masha ya awali na muziki

50 Cent alizaliwa mjini South Jamaica, Queens ndani ya New York, Marekani. 50 Cent ameanza kujishughulisha na masuala ya uuzaji wa dawa za kulevya toka akiwa na umri wa miaka 12, hiyo ilikuwa kwenye miaka ya '80', akiwa anajushughulisha na masuala ya uuzaji wa dawa za kulevya. 50 Cent pia akawa anajaribu kidogo masuala ya muziki wa rap na hip hop.

50 Cent alipigwa risasi tisa mnamo mwaka 2000. Kadri miaka inavyozidi kwenda 50 Cent akabahatika kutoa tepu ya nyimbo mchanganyiko ilyokuwa inaitwa "Guess Who's Back?" mnamo mwaka wa 2002.

50 Cent aligunduliwa kipaji chake na mwanamuziki 'Eminem' na kumwingiza katika studio ya Interscope Records kwa msaada wa Eminem na Dr. Dre, ambaye ndiye aliye tayarisha albamu ya kwanza ya 50 Cent na kumpa mafanikio makubwa katika ulimwengu wa muziki.

Remove ads

Studio binafsi

Mnamo mwaka 2003 50 Cent alianzisha Studio yake iitwayo G-Unit Records, ambayo iliingiza Marapa maarufu kama vile Young Buck, Lloyd Banks, na Tony Yayo, kitu ambacho kilipelekea kupata uhasama na chuki nzito na baadhi ya wasanii nchini marekani, moja kati ya wasanii hao ni Ja Rule, The Game, na Fat Joe. Pia 50 Cent alikuwa akiibia masuala ya uigizaji na kuonekana kwenye baadhi ya filamu zenye kuhusu albamu yake na filamu illitwa "Get Rich or Die Tryin" na akashiriki pia kwenye filamu ya "Iraq War" na filamu ya "Home of the Brave" iliyotoka mwaka 2006.

Remove ads

Albamu alizotoa

Filamu alizotoa

Maelezo zaidi Mwaka, Jina la Filamu ...
Remove ads

Tuzo alizopata

Viungo vya nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads