Shady Records

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Shady Records ni studio ya kurekodi muziki kutoka nchini Marekani. Studio ilianzishwa na Eminem na meneja wake Paul Rosenberg mwaka 1999 baada ya mafanikio makubwa ya albamu ya Eminem The Slim Shady LP.[1]

Ukweli wa haraka Shina la studio, Imeanzishwa ...

Mwaka wa 2006, Shady ilitoa albamu iliyokwenda kwa jina la Eminem Presents: The Re-Up. Albamu hii ilishirikisha wasanii ambao walikuwa miongoni mwa washirika wa mwanzo wa lebo hiyo. Shady Records pia iliandaa nyimbo zilizotumika kwenye filamu iliyoigizwa na Eminem, 8 Mile. Wimbo wa "Lose Yourself" ulitumika kwenye filamu hii na ni wimbo wa kwanza wa hip hop kupokea Tuzo ya Akademi kwenye kipengele cha wimbo bora.

Washirika wa sasa wa Shady records ni pamoja na Eminem, Bad Meets Evil, Westside Boogie na Grip, wakati washirika wa zamani ni pamoja na D12, Obie Trice, 50 Cent, Stat Quo, Bobby Creekwater, Cashis, Slaughterhouse, Yelawolf, Griselda, Westside Gunn na Conway the Machine.

Remove ads

Historia

2000–2004: Kuanzishwa, ukuaji na ugomvi

Thumb
Eminem alianzisha Shady Records mwaka wa 1999.

Baada ya Eminem kutoa albamu yake ya "The Slim Shady LP", alianzisha studio yake ya kurekodi muziki mwishoni mwa mwaka 1999. Eminem alikuwa anatafuta njia ya kutoa kazi za D12, na Rosenberg alikuwa na shauku ya kuanzisha lebo, hii ilipelekea wawili hao kuungana na kuanzisha Shady records.[2]

D12 ni wasanii wa kwanza kusainiwa na Shady kwani walikuwa wakiimba pamoja tangu miaka ya 1990, na washiriki walikuwa wamewekeana ahadi kwamba yeyote atakaye kuwa wa kwanza kufanikiwa angerudi na kuwasaini wenzake. [3] Mnamo Juni 2001, D12 ilitoa albamu ya "Devil's Night", na kushika nafasi ya 1 kwenye Billboard 200. [4] Obie Trice alitambulishwa na Bizzarre wa D12 kwa Eminem. Eminem alimsaini mnamo Juni 2001 kama msanii wa pili wa Shady.[5][6] Obie Trice alianza kupata umaarufu baada ya kufanya mitindo huru kwenye albamu ya Devil's Night.

Wakati akifanya maandalizi ya filamu ya 8 Mile, Eminem alikutana na 50 Cent. Eminem alikuwa amesikiliza nyimbo za awali za 50 Cent, akazipeleka kwa Dr. Dre na kumpa nafasi ya kufanya kazi pamoja kuendeleza kipaji chake. 50 Cent alikua msanii wa kwanza kusainiwa na Shady na Aftermath.[7] 8 Mile soundtrack ilikuwa albamu ya pili kutolewa na Shady.[8][9] Wimbo wa kwanza ulikuwa "Lose Yourself", wimbo huo ulichaguliwa kugombania tuzo mbalimbali na kufanikiwa kushinda Tuzo ya Akademi, ilikuwa mara ya kwanza kwa wimbo wa hip hop kushinda tuzo hiyo.[10][11][12] Wimbo wa pili ulikuwa "Wanksta" wa 50 Cent, ulipata maarufu sana katika mji wa nyumbani wa 50 Cent. [13] Wakati huu, Eminem pia alikuwa ameingia makubaliano na DJ Green Lantern, ambaye alitoa kanda mseto ya kwanza ya lebo hiyo, Invasion!, mwaka wa 2002.[14] Alikuwa DJ wa Eminem wakati wa Anger Management Tour. [15]

Remove ads

Wasanii

Wasanii wa sasa

Maelezo zaidi Msanii, Mwaka aliosainiwa ...

Wasanii wa zamani

Maelezo zaidi Msanii, Mwaka aliosainiwa ...
Remove ads

Diskografia

Albamu zote kwenye orodha ifuatayo zilizotolewa kupitia Shady Records na kusambazwa na Interscope Records. Studio yoyote ya ziada inayohusika imebainishwa.

Thumb
Kundi la Eminem, D12 limetoa albamu mbili kwenye lebo.
Thumb
Obie Trice alitoa albamu mbili kwenye lebo hii, kabla ya kuachana na Shady mwaka wa 2008.

Albamu za studio

Maelezo zaidi Msanii, Albamu ...

Albamu za mkusanyiko

Maelezo zaidi Msanii, Albamu ...

Extended plays

Maelezo zaidi Msanii, Albamu ...
Remove ads

Tanbihi

Vingo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads