Abba Likano

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Abba Likano alikuwa mmonaki aliyefanya umisionari katika Ethiopia ya leo akaanzisha monasteri kati ya karne ya 5 na karne ya 6[1].

Ni kati ya kundi la Watakatifu Tisa wa Kanisa la Kiorthodoksi la Ethiopia wanaosemekana kukimbilia nchi hiyo kutoka sehemu mbalimbali za Dola la Roma[2] kutokana na dhuluma zilizofuata Mtaguso wa Kalsedonia (451). Wengine ni Abba Panteleoni, Abba 'Aléf, Abba Gärima, Abba Guba, Abba Aftse, Abba Aregawi, Abba Sehma, Abba Yäm'ata (Yemata). Wote walikuwa wamonaki wasomi waliohuisha Ukristo wa Ethiopia. Wanasemekana kuwa ndio watafsiri wa Agano Jipya kwenda lugha ya Ge'ez.[3]

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 24 Novemba.

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads