Abba Sehma
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Abba Sehma alikuwa mmonaki aliyefanya umisionari katika Ethiopia ya leo akaanzisha monasteri chini ya kanuni ya Pakomi huko Sedenya[1].
Ni kati ya kundi la Watakatifu Tisa wa Kanisa la Kiorthodoksi la Ethiopia wanaosemekana kukimbilia nchi hiyo kutoka sehemu mbalimbali za Dola la Roma[2] kutokana na dhuluma zilizofuata Mtaguso wa Kalsedonia (451). Wengine ni Abba Panteleoni, Abba 'Aléf, Abba Gärima, Abba Guba, Abba Liqanos, Abba Aregawi, Abba Aftse, Abba Yäm'ata (Yemata). Wote walikuwa wamonaki wasomi waliohuisha Ukristo wa Ethiopia. Wanasemekana kuwa ndio watafsiri wa Agano Jipya kwenda lugha ya Ge'ez.[3]
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads