Abdel Fattah Abdelrahman Burhan
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Abdel Fattah Abdelrahman Burhan (kwa Kiarabu: عبد الفتاح عبد الرحمن البرهان ʿabd al-fattāḥ ʿabd ar-raḥmān al-burhān) ni mwanajeshi kutoka nchini Sudan aliyekuwa mwenyekiti wa Halmashauri ya Kijeshi ya Mpito tarehe 14 Aprili 2019 baada ya kupinduliwa kwa rais rais Omar al-Bashir na kujiuzulu kwa jenerali Ibn Auf kutoka Halmashauri ya Mpito. Katika nafasi hii amekuwa hali halisi mkuu wa dola la Sudan.[1].
'
Remove ads
Maisha ya awali
Burhan alizaliwa mnamo mwaka 1960 katika kijiji cha Gandatu upande wa kaskazini wa Khartoum. Burhan alisoma katika chuo cha kijeshi cha Sudan akaendelea pale Misri na Yordani. Ameoa ana watoto watatu.
Mwanajeshi
Alipanda ngazi jeshini katika vita za wenyewe kwa wenyewe kwenye Sudan Kusini, pia katika jimbo la Darfur. Aliendelea kuwa na vyeo vya uongozi katika jeshi na mwaka 2011 aliteuliwa kuwa mkuu wa jeshi la ardhi. Katika nafasi alisimamia pia vikosi vya Sudan vinavyoshiriki katika vita ya Saudia nchini Yemen tangu mwaka 2015. Mwezi wa Februari 2018 aliteuliwa na rais Bashir kuwa mkuu wa jeshi lote.[2].
Remove ads
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kijeshi ya Mpito
Baada ya kuwa mwenyekiti wa halmasahuri ya kijeshi Burhan alitangaza kuwa lengo la halmashauri yake ni kurudisha serikali ya kikatiba na kiraia. [3]
Tazama pia
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads