Adriano wa Nikomedia

From Wikipedia, the free encyclopedia

Adriano wa Nikomedia
Remove ads

Adriano wa Nikomedia (aliuawa 4 Machi 306)[1] alikuwa mkuu wa walinzi wa kaisari Galerius[1].

Thumb
Sanamu ya Mt. Adriano nchini Ufaransa.
Thumb
Picha takatifu ya Adriano na Natalia kutoka Urusi.

Alipokuwa na umri wa miaka 28, aliongokea Ukristo pamoja na mke wake Natalia[2], ilimbidi Adriano afie dini hiyo katika mji Nikomedia,[1][3] leo nchini Uturuki.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini. Kwa heshima yake Papa Honorius I aligeuza jengo la senati ya Roma kuwa kanisa[4].

Sikukuu yake huadhimishwa na Waorthodoksi katika tarehe tofauti; kwa Wakatoliki ni tarehe 8 Septemba.[5]

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads