Afrobeat

From Wikipedia, the free encyclopedia

Afrobeat
Remove ads

Afrobeat (pia inajulikana kama Afrofunk) ni aina ya muziki kutoka Afrika Magharibi unaochanganya athira kutoka katika muziki wa Kiyoruba, muziki wa Ghana (kama highlife), na athari kutoka kwa muziki wa Marekani kama funk, jazz, na soul.[1][2] Aina hii inajulikana kwa umakini wake kwa sauti za kuimbwa, midundo tata inayoshirikiana, na ngoma.[3] Mtindo huu wa muziki ulianzishwa katika miaka ya 1960 na mpiga vyombo kiongozi wa bendi kutoka Nigeria Fela Kuti, ambaye aliipa umaarufu ndani na nje ya Nigeria.

Afrobeat inatofautiana na Afrobeats, aina ya muziki inayochanganya sauti zinazotoka Afrika Magharibi katika karne ya 21. Hii inachukua athari kutoka kwa miziki kama hip hop, house, jùjú, ndombolo, R&B, soca, na dancehall.[4][5][6][7][8][9] Hizi mbili, ingawa mara nyingi hujikuta zikitatanishwa, si sawa.[5][6]

Thumb
Seun Kuti akiwa kwenye onyesho la Afrobeat[8]
Remove ads

Historia

Thumb
Fela Kuti

Afrobeat ilianza nchini Nigeria mwishoni mwa miaka ya 1960 na Fela Kuti (alizaliwa Olufela Olusegun Oludotun) ambaye, pamoja na mpiga ngoma Tony Allen, alijaribu mchanganyiko wa muziki wa kisasa wa wakati huo. Afrobeat ilijumuisha athari za aina mbalimbali za muziki, kama highlife, fuji, na jùjú,[10] pamoja na tamaduni za uimbaji, midundo, na vyombo vya Kiyoruba.[11] Mwishoni mwa miaka ya 1950, Kuti aliondoka Lagos kwenda kusoma nchini Uingereza katika Shule ya Muziki ya London, ambapo alipata masomo ya piano[12] na ngoma[13] na alijifunza muziki wa jazz. Fela Kuti alirejea Lagos na kuanzisha mchanganyiko wa muziki wa highlife na jazz, ingawa hakupata mafanikio ya kibiashara.[3]

Mnamo mwaka wa 1969, Kuti na bendi yake walifanya ziara nchini Marekani na kukutana na mwanamke aitwaye Sandra Smith, mwimbaji na mhamasishaji wa Black Panther Party. Sandra Smith (ambaye sasa anajulikana kama Sandra Izsadore au Sandra Akanke Isidore) alimwonyesha Kuti maandiko ya wanaharakati kama Martin Luther King Jr., Angela Davis, Jesse Jackson, na mtu aliyeathiri sana Fela, Malcolm X.[5]

Kama Kuti alivyokuwa na hamu na siasa za Wamarekani Weusi, Smith alifanya jitihada kumjulisha kuhusu matukio ya sasa; kwa upande wake, Kuti alimfundisha kuhusu tamaduni za Afrika. Kwa kuwa Kuti alikaa nyumbani kwa Smith na alitumia muda mwingi naye, alianza kutathmini tena aina ya muziki wake. Hapo ndipo Kuti aligundua kwamba hakuwa akicheza muziki wa Kiafrika. Tangu siku hiyo, Kuti alibadilisha sauti yake na ujumbe alionao katika muziki wake.[14]

Aliporudi Nigeria, Kuti alibadili jina la bendi yake kuwa "Africa 70," na akaanzisha sauti ya Afrobeat. Baada ya bendi yake kujulikana nchini Nigeria na Afrika Magharibi. Ukaazi wake na Smith, ulimfanya pia abadili kabisa muundo wa mashairi yake kutoka starehe hadi harakati za kupigania uhuru wa Afrika katika miaka ya 1970.[15]

Remove ads

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads