Agnes Le Thi Thanh

From Wikipedia, the free encyclopedia

Agnes Le Thi Thanh
Remove ads

Agnes Le Thi Thanh (1781 - 1841) alikuwa Mkristo mama wa familia wa Vietnam aliyeteswa sana kwa sababu alificha padri fulani nyumbani mwake, hata hivyo alikataa kukana imani yake akafa gerezani chini ya kaisari Thieu Tri [1].

Thumb
Mt. Agnes alivyochorwa.

Ni mmojawapo kati ya Wakristo wafiadini wa Vietnam waliouawa kwa ajili ya imani yao huko Vietnam katika karne ya 17, 18 na 19 (16251886).

Wanatajwa pia kama Watakatifu Andrea Dũng-Lạc na wenzake 116.

Kwa nyakati tofauti, Papa Leo XIII, Papa Pius X na Papa Pius XII waliwatangaza kuwa wenye heri, halafu Papa Yohane Paulo II aliwaunganisha katika kuwafanya watakatifu wafiadini tarehe 19 Juni 1988.

Sikukuu yao huadhimishwa kwa pamoja kila tarehe 24 Novemba, lakini ya kwake mwenyewe tarehe 12 Julai[2].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo ya Kiswahili

Marejeo ya lugha nyingine

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads