Ahazi

From Wikipedia, the free encyclopedia

Ahazi
Remove ads

Ahazi (kwa Kiebrania אָחָז, ʼAḥaz; kwa Kigiriki: Ἄχαζ, Ἀχάζ, Akhaz; kwa Kilatini: Achaz;[1] kifupisho cha Jehoahaz, יְהוֹאָחָז, Yəhō’aḥaz, Yehō’aḥaz)[2] alikuwa mfalme wa Yuda, mtoto na mrithi wa Yothamu tangu mwaka 732 KK hadi 716 KK[3][4].

Thumb
Ahazi katika Promptuarii Iconum Insigniorum, kazi ya Guillaume Rouillé (1553).

Ahazi anachorwa kama mtu mbaya katika Kitabu cha Pili cha Wafalme (16:2), Kitabu cha Isaya 7-9 na Kitabu cha Pili cha Mambo ya Nyakati 28.

Alitabiriwa na nabii Isaya kwamba mwanamwali atamzalia mtoto wa kiume atakayethibitisha uwepo wa Mungu pamoja na watu wake, jina lake Emanueli litakavyomaanisha. (7:1-17) Kweli mke wa Ahazi alimzaa Hezekia atakayeendeleza ufalme wa ukoo wa Daudi, lakini Wakristo wanaona utabiri huo ulimlenga zaidi Yesu, mwana wa Bikira (walivyoelewa watafsiri wa kwanza wa Biblia katika Kigiriki) ambaye kweli ni Mungu pamoja nasi, na ni mwana wa Daudi ambaye atatawala milele kwa amani na haki (11:1-9).

Kwa kukosa imani katika msaada huo wa Mungu Ahazi aliwaita Waashuru na hivyo kuchangia mangamizi ya Ufalme wa Israeli (Kaskazini)[5] .

Injili ya Mathayo inamtaja katika orodha ya vizazi vya Yesu.

Remove ads

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads