Ajilo
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Ajilo (pia: Agilus, Agile, Aile, Ayeul, El; Burgundy, leo nchini Ufaransa, 580 hivi – Rebais, Ufaransa wa leo, 650 hivi) alikuwa abati wa kwanza wa monasteri ya Rebais kuanzia mwaka 636 hadi kifo chake.
Alipoingia utawani huko Luxeuil akiwa bado mtoto, mwalimu wake alikuwa Kolumbani. Baada ya kupata upadirisho alifanya kwa mafanikio umisionari huko Bavaria pamoja na Eustasi wa Luxeuil[1].
Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads