Alfabeti
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Alfabeti ni kiasi cha alama zinazotumiwa kuandika sauti za lugha fulani. Alama hizi hupatikana kama orodha kwa ufuatano uliokubaliwa, kwa mfano katika Kiswahili:

Alfabeti: Kilatini , Kisirili , Kilatini pamoja na Kisirili , Kigiriki , Kigeorgia na Kiarmenia
Abjadi: Kiarabu , Kiarabu pamoja na Kilatini , Kiebrania pamoja na Kiarabu
Abugida: Kihindi ya Kaskazini , Kihindi ya Kusini , Kiethiopia , Kithaana Mwandiko wa kizalendo wa Kanada ,
Alama kwa neno lote na alama za silabi: Alama za neno lote , Mchanganyiko wa alama za maneno na silabi , Mchanganyiko alfabeti na silabi Mchanganyiko alfabeti na silabi
"a, b, ch, d, dh, e, f, g, gh, h, i, j, k, kh, l, m, mb, mv, n, nd, ng, ng', nj, ny, nz, o, p, r, s, sh, t, th, u, v, w, y, z"
Jina la "alfabeti" hutokana na mwandiko wa Kigiriki ambamo herufi mbili za kwanza ni α "alfa" na β "beta".
Alfabeti ni mtindo wa mwandiko uliosambaa duniani kote. Kwa lugha nyingi imechukua nafasi ya miandiko ya awali.
Alfabeti huonyesha sauti si maneno kamili - hii ni tofauti na mwandiko kama Kichina wenye alama kwa ajili ya neno lote.
Remove ads
Alfabeti inayotumiwa zaidi kimataifa ni alfabeti ya Kilatini (au "alfabeti ya Kirumi"). Lakini kuna alfabeti nyingine kadhaa zinazojulikana kimataifa kama vile:
- Alfabeti ya Kigiriki hutumiwa kwa lugha ya Kigiriki.
- Alfabeti ya Kiarabu hutumiwa kwa Kiarabu, Kiajemi na Kiurdu.
- Alfabeti ya Kiebrania hutumiwa kwa Kiebrania na Kiyidish.
- Alfabeti ya Kisirili hutumiwa kwa lugha za Kislavoni kama Kirusi, Kibulgaria, Kiserbia na pia lugha za Asia ya Kati.
Mengine ni alfabeti kama vile ya Kikopti, ya Kigeorgia, ya Kiarmenia n.k.
Remove ads
Aina za pekee za alfabeti ni miandiko ya "abugida". Hii inamaanisha namna ya kuandika ambako hakuna alama za pekee kwa ajili ya vokali. Kila alama ya konsonanti ina namna mbalimbali ya kuonekana kwa kuongeza alama ndogo inayoonyesha ni vokali ipi inayofuata. Mifano yake ni:
- Alfabeti ya Kiethiopia
- Devanagari au alfabeti ya Kihindi
Viungo vya nje
- Rhonda L. Hartell, Alphabets de Langues Africaines (Swahili: page 177) (Kifaransa)
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads