Alfege wa Canterbury

From Wikipedia, the free encyclopedia

Alfege wa Canterbury
Remove ads

Alfege wa Canterbury (jina lake huandikwa pia “Aelfheah”; takriban 954 19 Aprili 1012) alikuwa mkaapweke, halafu abati wa monasteri, askofu na hatimaye askofu mkuu wa Canterbury nchini Uingereza.

Thumb
Mt. Alfege.

Mwaka 1011, wakati wa uvamizi wa kikatili wa maharamia Wadenmark, alijitoa badala ya waumini wake akakamatwa, na kwa kuwa alikataa kukombolewa kwa pesa, Jumamosi baada ya Pasaka alipigwa kwa mifupa ya kondoo na hatimaye alikatwa kichwa kwenye kingo ya mto Thames, karibu na Greenwich[1].

Alitambuliwa rasmi kuwa mtakatifu mfiadini na Papa Gregori VII mwaka 1078.

Sikukuu yake ni tarehe 19 Aprili[2].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads