Pasaka

From Wikipedia, the free encyclopedia

Pasaka
Remove ads

Pasaka ni sikukuu muhimu katika dini za Uyahudi na Ukristo. Jina la Pasaka limetokana na neno la Kiebrania "פסח" (tamka: pasakh).

Thumb
Meza ya Seder yaani Chakula cha Pasaka ya Kiyahudi ikionyesha vitabu vya Haggada.
Thumb
Yesu mfufuka.
Thumb
Mayai ya Pasaka.

Aina

Taarifa za Agano Jipya zinatoa habari ya kuwa kufa na kufufuka kwa Yesu yametokea wakati wa sikukuu ya Pasaka ya Kiyahudi. Kwa hiyo jina la sikukuu hiyo limeendelea kutumika kwa ajili ya sherehe ya Kikristo.

Remove ads

Tarehe ya Pasaka

Katika kalenda ya kawaida tarehe ya Pasaka inabadilika kila mwaka, ila inapatikana katika Machi au Aprili tu, kwa sababu upande mmoja inafuata kuonekana kwa mwezi angani, lakini imefungwa pia kwa sikusare (au ekwinoksi, yaani siku ya usawa wa mchana na usiku), kwa hiyo haizunguki mwaka mzima kama tarehe za sherehe za Uislamu.

Pasaka ya Kiyahudi inafuata kalenda yao maalumu: ni tarehe 15 Nisan ambayo ni siku baada ya mwezi mpevu wa kwanza unaofuata sikusare ya Majira ya machipuko katika nusutufe ya kaskazini ya Dunia (mnamo 21 Machi).

Wakristo wa kwanza, ambao wote walikuwa Wayahudi, walisherehekea sikukuu ya Kiyahudi pamoja na kumbukumbu ya ufufuko wa Yesu. Baadaye sherehe na pia tarehe zikawa tofauti, ingawa bila kwenda mbali sana.

Badiliko kubwa zaidi lilikuwa lile la Wakristo, tangu karne ya 1 au ya 2, kuadhimisha daima Pasaka siku ya Jumapili kwa kuwa ndiyo siku ya ufufuko, wakati Wayahudi wanaadhimisha Pasaka kwa kuangalia tarehe, bila kujali ni siku ipi ya juma.

Mtaguso wa kwanza wa Nisea mwaka 325 uliamua kwamba Pasaka isherehekewe Jumapili ya kwanza baada ya mwezi mpevu wa kwanza unaofuata tarehe 21 Machi. Kwa kuwa mwezi mpevu baada ya 21 Machi inaweza kutokea kati ya 22 Machi na 19 Aprili, tarehe ya Pasaka, ambayo ni Jumapili inayofuata, hutokea kati ya 22 Machi na 25 Aprili.

Katika Ukristo kuna kalenda mbili zinazotumika, hivyo pia tarehe mbili za Pasaka. Kanisa la magharibi, yaani Wakatoliki wengi na Waprotestanti, hufuata kalenda ilivyorekebishwa na Papa Gregori XIII (ambayo imekuwa kalenda ya kawaida ya kimataifa), lakini Waorthodoksi wanaendelea kutumia kalenda iliyotangulia, yaani Kalenda ya Juliasi. Ndiyo maana mara nyingi Pasaka inaadhimishwa katika Jumapili tofauti kati ya pande hizo mbili: tofauti ya kalenda inaleta Kanisa la Mashariki kusheherekea Pasaka wakati mwingine hata katika mwezi Mei wa kalenda ya Gregori, kwa kuwa kwao bado ni Aprili kufuatana na kalenda ya Juliasi.

Kwa sasa kuna majadiliano yenye lengo la kukubaliana ili kuadhimisha Pasaka pamoja kama ilivyokusudiwa na Mtaguso wa kwanza wa Nisea.

Remove ads

Majina ya Pasaka katika lugha mbalimbali

Katika lugha nyingi, asili hii bado inaonekana, ingawa mara nyingi umbo la neno ni tofauti kidogo. Jina la sikukuu ya Kiyahudi linapatikana kwa maumbo mbalimbali. Siku hizi mara nyingi umbo la neno la Kiebrania limetumika lakini desturi katika lugha hizo inaonyesha pia umbo linalofanana zaidi na neno kwa ajili ya sherehe ya Kikristo.

Maelezo zaidi Lugha, Jina la Pasaka ya Kiyahudi ...

Viungo vya nje

Ukweli wa haraka

Liturujia

Desturi

Hesabu

Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Remove ads
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads