Kiamhari
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Kiamhari (kwa Kiingereza Amharic) ni lugha ya Kisemiti inayozungumzwa hasa nchini Ethiopia, ambapo ni lugha rasmi ya taifa. Ni lugha ya pili kwa ukubwa wa wasemaji wa lugha za Kisemiti baada ya Kiarabu. Kiamhari hutumia mfumo wa maandishi wa Ge'ez (Fidel), ambao ni hati badala ya alfabeti ya kawaida, ambapo kila ishara huwakilisha silabi. Kwa sasa, Kiamhari kinazungumzwa na zaidi ya 32 milioni kama lugha ya kwanza na na wengine takriban 25 milioni kama lugha ya pili.
"am" inaelekezwa hapa. Kwa matumizi mengine, tazama am (maana).
Lugha hii ina historia ndefu na imekuwa lugha ya kifalme na serikali ya Ethiopia kwa karne nyingi.Ni lugha kuu ya serikali, elimu, vyombo vya habari, na biashara nchini Ethiopia. Kiamhari pia kina maneno mengi yaliyokopwa kutoka Kiarabu, Kiitaliano, na Kiingereza kutokana na mwingiliano wa kihistoria na mataifa mengine. Licha ya Kiswahili kuwa lugha pana zaidi barani Afrika, Kiamhari kinabakia kuwa mojawapo ya lugha chache za Kiafrika zilizo na mfumo wake wa maandishi unaojitegemea.
Remove ads
Chati ya Kiamhari
Remove ads
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads