Kiitalia

From Wikipedia, the free encyclopedia

Kiitalia
Remove ads

Kiitalia ("lingua italiana" au "italiano") ni lugha ya kirumi katika lugha za Kihindi-Kiulaya na ndiyo iliyo karibu sana na lugha ya Kilatini.Ikiwa na wasemaji milioni 85 ambao Milioni 67 kama lugha ya mama ni lugha ya 21 kubwa zaidi duniani.Ni lugha rasmi ya Italia, San Marino, Vatikano, Uswisi na katika sehemu za Slovenia na Kroatia.Inatumika pia katika Monako, Malta, Albania na visiwa kadhaa vya Ugiriki), halafu bado katika elimu katika nchi zilizokuwa makoloni ya Italia kama Eritrea, Libya, Ethiopia na Somalia.

Ukweli wa haraka Kiitalia Italiano (it), Lugha ...
Thumb
Dante Alighieri (juu) na Petrarca (chini) walichangia sana kufanya lahaja ya Firenze ienee kuanzia karne za kati
Thumb
Thumb
Pietro Bembo alisanifu lugha ya Kiitalia kwa kutegemea lahaja ya Toscana

Watu wengi wanaokitumia kama lugha mama wamekisambaza katika nchi zote walikohamia, kama vile Ujerumani, Ufaransa, Ubelgiji, Marekani, Kanada, Brazil, Uruguay, Argentina, Venezuela, Australia n.k.[1]

Ni ya 4 kati ya lugha za kigeni zinazosomwa zaidi duniani, hasa kwa sababu ya umuhimu wake katika ustaarabu, kuanzia muziki, lakini pia katika biashara, k.mf. ya bidhaa za utamaduni wa Italia.

Kihistoria asili yake ni lugha ya Kilatini, hivyo pamoja na Kifaransa, Kihispania, Kireno, Kiromania na lugha nyingine ndogo ni moja ya lugha za Kirumi. Kati ya lugha hizo, Kiitalia ndicho kinachofanana zaidi na Kilatini, labda baada ya Kisardinia.

Imegawanyika katika lahaja nyingi, hasa za Kaskazini na za Kusini mwa rasi hiyo. Imesanifiwa kwa msingi wa lahaja ya Firenze (mkoa wa Toscana, Italia ya Kati).

Remove ads

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads