Amoni, Zeno na wenzao
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Amoni, Zeno na wenzao Tolomayo, Ingene na Theofilo (walifia dini Aleksandria, Misri, 249 hivi) wakati wa dhuluma ya kaisari Decius.
Habari zao zinapatikana katika Historia ya Kanisa iliyoandikwa na Eusebi wa Kaisarea akiripoti barua ya Dionisi wa Aleksandria kwa Fabio wa Antiokia [1].
Theofilo alikuwa mzee, wengine wanne askari; wakiwa mahakamani wakati Mkristo mwenzao alipokuwa anateswa ili aache imani, walikuwa wanamtia moyo asizidi kuyumba kutokana na maumivu makali. Hapo umati uliwapigia kelele, nao wakajitosa katikati kujitangaza Wakristo wakauawa mara moja [1][2][3].
Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama watakatifu wafiadini[4][2][5] .
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Marejeo ya lugha nyingine
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads