Ana (nabii)
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Ana (kwa Kiebrania חַנָּה, Hannah, kwa Kigiriki Ἄννα, Anna) alikuwa mwanamke wa karne ya 1 KK katika Israeli.

Ni maarufu kama nabii kutokana na habari iliyomo katika Injili ya Luka (2:36-38[1]).
Humo tunaambiwa kwamba alikuwa binti Fanueli, wa kabila la Asheri.
Alipoachwa mjane ujanani baada ya miaka 7 ya ndoa, alihamia hekalu la Yerusalemu akifunga chakula na kusali hadi miaka 84.[2][3][4][5][6][7][8]
Mtoto Yesu alipoletwa hekaluni siku 40 tu baada ya kuzaliwa, Ana alitangaza habari zake kwa waliokuwepo [9].
Tangu kale anaheshimiwa na madhehebu mengi ya Ukristo kama mtakatifu nabii.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 3[10] au 16 Februari.[11][12]
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads