Andrea Avellino
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Andrea Avellino (Castronuovo di Sant'Andrea, Potenza, 1521 – Napoli, 10 Novemba 1608), alikuwa padri wa Italia[1] wakati wa Urekebisho wa Kikatoliki akajiunga[2] na aina mpya ya utawa aliyoianzisha Gaetano wa Thiene, maarufu kwa jina la Wateatini, akaieneza zaidi pamoja na kufanya utume.

Pamoja na kung'aa kwa maisha matakatifu na juhudi kwa wokovu wa wengine, alijifunga kwa nadhiri ngumu ya kupiga hatua kila siku kuelekea ukamilifu wa Kikristo, na hatimaye, akiwa mwingi wa stahili, alifariki altareni.[3].
Alitangazwa na Papa Urban VIII kuwa mwenye heri tarehe 14 Oktoba 1624, halafu Papa Klementi XI alimtangaza mtakatifu tarehe 22 Mei 1712.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads