Milano
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Milano (pia Milan) ni mji mkubwa wa Italia ya kaskazini wenye wakazi milioni 1.3. Rundiko la mji lina wakazi milioni 7.5. Ni mji mkuu wa mkoa wa Lombardia na kitovu cha uchumi na utamaduni.

Remove ads
Historia
Mji ulianzishwa mnamo 400 KK na Wakelti ukawa mji wa Kiroma mnamo 222 KK ukajulikana kama Mediolanum. Mji ulikua katika Dola la Roma. Mwaka 293 Kaisari Diokletiano alichagua Milano kama mji mkuu wa nusu ya magharibi ya Dola la Roma. Tamko la Milano lilitolewa huko mwaka 313 na makaisari Licinius na Konstantino Mkuu likatangaza mwisho wa mateso ya Wakristo.
Baada ya mwisho wa Dola la Roma Magharibi mji uliharibiwa mara mbili na Wahunni na Waostrogoti wakati wa uhamisho wa Wajerumaniki. Ukatekwa tena na Walombardi wahamiaji na kuwa mji mkuu wao. Mwaka 774 uliingizwa katika himaya ya Karolo Mkuu ukaendelea kama sehemu ya falme za Wafaranki, Wajerumani na Habsburg kwa karne nyingi.
Katika karne ya 19 wenyeji walidai kujitawala kama Waitalia na baada ya vita ya Ufalme wa Sardinia na Ufaransa dhidi ya Austria Lombardia yote ikawa sehemu ya ufalme wa Sardinia-Piemonte ulioendelea na kuwa Ufalme wa Italia.
Katika Italia mpya Milano ulikuwa kitovu cha uchumi. Ujenzi wa reli ulianzisha upanuzi wa viwanda. Milano ikawa mji wa viwanda na kukua haraka. Baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia Benito Mussolini alianzisha harakati ya Ufashisti mjini Milano.

Remove ads
Umuhimu wa Milano katika Italia
Leo hii Milano ni mji wa pili katika Italia. Benki kubwa za nchi zina makao makuu hapa, pia soko la hisa la Italia. Kuna viwanda vingi pamoja na kampuni ya magari ya Alfa Romeo na kampuni ya matairi Pirelli. Pia mji huu ni makao makuu ya vyombo vya habari mbalimbali kama Mediaset na magazeti kama Il Corriere della Sera. Mji huu pia ni kitovu cha michezo mbalimbali. Una uwanja wa Giuseppe Meazza (San Siro) wenye uwezo wa kubeba watazamaji zaidi ya 80,000 ambao ndio mkubwa kuliko vyote nchini Italia. Pia kuna timu mbili za mpira wa miguu, Internazionale na AC Milan ambazo ni kati ya vilabu vinavyoheshimika duniani. Milano huitwa mji mkuu wa mitindo ya mavazi ya Italia.
Mji unajulikana sana kwa ukumbi wake wa opera unaoitwa "Scala". Jengo mashuhuri zaidi ni kanisa kuu au "duomo".
Remove ads
Viungo vya nje
- Tovuti rasmi Ilihifadhiwa 15 Juni 2001 kwenye Wayback Machine. (Kiitalia)
![]() |
Makala hii kuhusu maeneo ya Italia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Milano kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads