Andrea Nguyen Kim Thong
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Andrea Nguyen Kim Thong (1790-1855) alikuwa katekista wa Vietnam ambaye, kisha kukaa gerezani chini ya kaisari Du Tuc, alihukumiwa kwenda uhamishoni, lakini njiani alifariki akiwa amefungwa pingu na kutwishwa ubao mzito[1]

Ni mmojawapo kati ya Wakristo wafiadini wa Vietnam waliouawa kwa ajili ya imani yao huko Vietnam katika karne ya 17, 18 na 19 (1625–1886).
Wanatajwa pia kama Watakatifu Andrea Dũng-Lạc na wenzake 116.
Kwa nyakati tofauti, Papa Leo XIII, Papa Pius X na Papa Pius XII waliwatangaza kuwa wenye heri, halafu Papa Yohane Paulo II aliwaunganisha katika kuwafanya watakatifu wafiadini tarehe 19 Juni 1988.
Sikukuu yao huadhimishwa kwa pamoja kila tarehe 24 Novemba, lakini ya kwake mwenyewe tarehe 15 Julai[2].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Marejeo ya lugha nyingine
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads