Angela Merichi

From Wikipedia, the free encyclopedia

Angela Merichi

Angela Merichi (Desenzano, Brescia, 21 Machi 1474 – Brescia, 27 Januari 1540) alikuwa bikira wa kaskazini mwa Italia ambaye, akifuata kanuni ya Utawa wa Tatu wa Mt. Fransisko, alikusanya pamoja wasichana, ambao aliwafundisha kutenda matendo ya huruma.

Thumb
Mt. Angela Merichi

Mwaka 1535, huko Brescia, alianzisha shirika la Waursula, chama cha wanawake waliojishughulisha kuwafundisha wasichana maskini jinsi ya kuwa Wakristo wema [1].

Ametambuliwa na Papa Klementi XIII kuwa mwenye heri tarehe 30 Aprili 1768, halafu na Papa Pius VII kuwa mtakatifu tarehe 24 Mei 1807.

Sikukuu yake ni tarehe 27 Januari[2].

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.