Antonino Fantosati

From Wikipedia, the free encyclopedia

Antonino Fantosati
Remove ads

Antonino Fantosati (Trevi, Umbria, Italia, 16 Oktoba 1842 - Taiyuan, Shanxi, China, 7 Julai 1900) alikuwa mtawa wa shirika la Ndugu Wadogo na askofu mmisionari wa Kanisa Katoliki aliyeuawa kwa kupigwa mawe huku akijitokeza pamoja na padri Yosefu Maria Gambaro kutetea waumini wakati wa Uasi wa Waboksa nchini China[1].

Thumb
Picha yake halisi.

Alitangazwa na Papa Pius XII kuwa mwenye heri tarehe 27 Novemba 1946.

Anaheshimiwa na Kanisa hilo kama mtakatifu mfiadini tangu tarehe 1 Oktoba 2000, alipotangazwa na Papa Yohane Paulo II pamoja na wenzake 119 maarufu kama wafiadini wa China.

Sikukuu yao huadhimishwa kwa pamoja kila mwaka tarehe 9 Julai, lakini ya kwake mwenyewe tarehe ya kifodini chake[2].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads