Aretha mfiadini
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Aretha (kwa Kiarabu: الحارث, "al-Haarith") alikuwa kiongozi wa Wakristo Waorthodoksi wa Mashariki wenye asili ya Ethiopia walioishi Najran (leo Ukhdūd nchini Saudia) mwanzoni mwa karne ya 6, wakati wa kaisari Yustino.

Aliuawa pamoja na wenzake walau 340, kama si 4,000 au 20,000[1] (akiwemo mke wake Ruma na mabinti wao wanne) mwaka 523, wakati wa dhuluma ya mfalme Dhu Nuwas aliyekuwa ameongokea dini ya Uyahudi .[2][3]
Anajulikana kupitia Acta S. Arethae (pia: Martyrium sancti Arethae au Martyrium Arethae)[4][5][6]
Kurani inalaani dhuluma hiyo katika sura LXXXV:4-8.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu mfiadini[7].
Sikukuu yake na ya wenzake huadhimishwa nao tarehe 24 Oktoba[8][9].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads