Atala wa Bobbio

From Wikipedia, the free encyclopedia

Atala wa Bobbio
Remove ads

Atala wa Bobbio (Burgundy, karne ya 6 - Bobbio, Italia, 10 Machi 627) alikuwa mmonaki kutoka Ufaransa wa leo anayejulikana hasa kama mfuasi wa Kolumbani huko Luxeuil, alipohamia kutoka monasteri ya Lerins ili kupata maisha magumu zaidi.

Thumb
Mt. Atala.

Baada ya kufukuzwa nchini (612), walianzisha monasteri mpya huko Bobbio (614) ambayo baada ya mwaka mmoja ilibaki chini yake kutokana na kifo cha Kolumbani (615).

Aliongoza kwa ari na utambuzi hivi kwamba chini yake monasteri hiyo ikastawi sana pamoja na kuvuta Walombardi Waario katika Kanisa Katoliki[1].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 10 Machi[2].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads