Augustino Schoeffler
shahidi wa Ufaransa na mtakatifu From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Augustino Schoeffler, M.E.P. (1822 - 1851) alikuwa padri wa Ufaransa aliyefanya umisionari nchini Vietnam miaka mitatu hadi alipokamatwa, kufungwa na kukatwa kichwa kwa amri ya kaisari Tu Duc kwa sababu ya dini yake, akawa hivyo mfiadini kama alivyokuwa akiomba sikuzote [1].

Ni mmojawapo kati ya Wakristo wafiadini wa Vietnam waliouawa kwa ajili ya imani yao huko Vietnam katika karne ya 17, 18 na 19 (1625–1886).
Wanatajwa pia kama Watakatifu Andrea Dũng-Lạc na wenzake 116.
Kwa nyakati tofauti, Papa Leo XIII, Papa Pius X na Papa Pius XII waliwatangaza kuwa wenye heri, halafu Papa Yohane Paulo II aliwaunganisha katika kuwafanya watakatifu wafiadini tarehe 19 Juni 1988.
Sikukuu yao huadhimishwa kwa pamoja kila tarehe 24 Novemba, ila ya kwake menyewe tarehe 1 Mei[2].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Marejeo ya lugha nyingine
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads