Baali

From Wikipedia, the free encyclopedia

Baali
Remove ads

Baali (maana yake mmiliki au Bwana katika lugha za Kisemiti za Kaskazini zilizotumika huko Mashariki ya Kati ya kale) ni jina lililokuja kutumika kwa ajili ya miungu, hasa kwa mungu wa dhoruba na wa uzazi, Hadad.

Thumb
Sanamu yake ya mwaka 1500 KK hivi.

Biblia ya Kiebrania inalitumia mara 90 kuhusiana na miungu mbalimbali ya makabila jirani na Waisraeli waliosadiki Mungu mmoja tu na kuona hiyo mingine kuwa miungu bandia tu. Biblia inaeleza ibada za makuhani wa Baali [1], na hasa shindano lililoitishwa na nabii Eliya juu ya mlima Karmeli ili kuwaonyesha Waisraeli yupi ni Mungu wa kweli kati ya YHWH na Baali dhidi ya juhudi za malkia Jezebeli za kueneza kati yao dini ya taifa lake (Tiro) [2].

Matumizi hayo yaliingia katika Ukristo[3] na Uislamu[4], pengine kwa umbo la dharau Beelzebub, kuhusu pepo.

Remove ads

Tanbihi

Marejeo

Marejeo mengine

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads