Bahasha

From Wikipedia, the free encyclopedia

Bahasha
Remove ads

Bahasha ni mfuko unaopokea na kuhifadhi barua ndani yake. Kwa kawaida hutengenezwa kwa karatasi iliyokunjwa na kushikwa kwa gundi.

Thumb
Bahasha; rangi zake zinaonyesha ya kwamba iliandaliwa kwa barua itakayopelekwa kwa ndege; alama nyekundu inaonyesha msimbo wa posta unaotumiwa kama sehemu ya anwani

Maandishi ya bahasha

Bahasha inaweza kutumiwa bila maandishi kama barua inafikishwa na mwandishi moja kwa moja kwa mpokeaji.

Lakini kwa kawaida kwenye huduma za posta bahasha inatakiwa kuwa na

Aina za bahasha

Kuna aina nyingi za bahasha zinazouzwa. Ukubwa hufuata kwa kawaida fomati za karatasi; katika nchi nyingi ni fomati za ISO 216 na barua nyingi kutumia karatasi za A4 na bahasha zinazoendana na ukubwa huu mara nyingi fomati za C6 kama karatasi inakunjwa hadi C4 kama haikunjwi.

Kwa kurahisisha kazi kuna bahasha yenye dirisha ambamo anwani inaonekana kama inaandikwa mahali sahihi kwenye barua; dirisha inaruhusu kuonekana kwa anwani pekee.

Kwa yaliyomo yenye thamani kuna pia bahasha ambazo zimeimarishwa.

Remove ads

Bahasha na siri ya barua

Bahasha inaweza kufungwa, na katika sheria za nchi nyingi bahasha iliyofungwa inatakiwa kufunguliwa tu na mpokeaji wa barua; wengine wanaobeba barua au kuipata kwa niaba ya wengine tu hawaruhusiwi kuifungua. Hata polisi au vyombo vingine vya serikali haviruhusiwi, isipokuwa kwa amri ya mahakama kufuatana na sheria za nchi.

Historia ya bahasha

Thumb
Kigae cha mwandiko wa kikabari pamoja na bahasha yake ya udongo uliokaushwa; takriban mwaka 2037 KK.

Kiasili neno "bahasha" lilimaanisha mfuniko, gunia, sanduku au namna nyingine ya kufunika kitu ndani yake. [1]

Bahasha za barua zimekuwa kawaida tangu karne ya 19 pamoja na kuboreshwa kwa huduma za posta na upatikanaji wake kwa watu wengi. Mwaka 1845 mashine ya kwanza ya kutengezea bahasha ilirekodiwa nchini Uingereza chini ya sheria ya hataza[2].

Bahasha zilipatikana pia zamani lakini hazikuwa kawaida jinsi ilivyokuwa baadaye. Kuna mifano ya bahasha za udongo wa mfinayanzi kwa ajili ya barua zilizoandikwa kwenye vigae vya mwandiko wa kikabari zamani za Babeli. Wachina, waliokuwa watu wa kwanza kugundua karatasi, walitengeneza pia mifuko au bahasha za karatasi. Lakini mara nyingi karatasi au ngozi ambamo barua iliandikwa iliviringishwa tu na labda kufunikwa katika kitambaa kwa kuilinda.

Remove ads

Tanbihi

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads