Barbara Ko Suni
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Barbara Ko Suni (Seoul, 1798 - Seoul, 29 Desemba 1839) alikuwa mwanamke mwenye familia wa Korea ambaye, pamoja na wenzake sita (Benedikta Hyong Kyongnyon, Barbara Cho Chungi, Magdalena Han Yongi, Petro Choe Changhub, Elizabeti Chong Chonghye na Magdalena Yi Yongdok), kisha kuteswa sana kwa ajili ya jina la Kristo, alikatwa kichwa [1].
Ni mmojawapo katika kundi kubwa la Wakristo wa Kanisa Katoliki nchini Korea waliouawa kwa ajili ya imani yao katika miaka 1791–1888. Wanakadiriwa kuwa 8,000 - 10,000.
Yeye na wenzake 102 walitangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa watakatifu tarehe 6 Mei 1984.[2]
Sikukuu ya hao Wafiadini wa Korea huadhimishwa tarehe 20 Septemba, lakini ya kwake mwenyewe tarehe 29 Desemba[3].
Remove ads
Mazingira
Mwishoni mwa karne ya 18, Ukristo wa Kikatoliki ulianza kuenea taratibu nchini[4] kwa juhudi za wananchi walei. Mwaka 1836 Korea, nchi ya Kikonfusyo ilipata wamisionari wa kwanza kutoka nje (wanashirika wa Paris Foreign Missions Society)[5].
Chini ya nasaba ya Joseon, Ukristo ulifutwa, tena waamini walidhulumiwa na kuuawa. Waliobaki walipaswa kushika imani yao kwa siri.
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Marejeo ya lugha nyingine
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads