Bartolomea Capitanio

From Wikipedia, the free encyclopedia

Bartolomea Capitanio
Remove ads

Bartolomea Capitanio (13 Januari 1807 - 26 Julai 1833) alikuwa mwanamke bikira wa Italia kaskazini ambaye, pamoja na Visensya Gerosa, alianzisha shirika la Masista wa Upendo wa Lovere, ambao kwa kawaida wanaitwa Masista wa Maria Mtoto.

Thumb
Mt. Bartolomea alivyochorwa.

Maisha

Bartolomea alizaliwa katika kijiji cha Lovere, mkoani Lombardia.

Alipokutana na Visensya waliungana kupambana na ujinga na ufukara wa watu wa eneo lao.

Mwaka 1833 walisaini hati ya kuanzisha shirika, ila baada ya miezi tu alifariki kwa ugonjwa wa kifua kikuu lakini hasa kwa kuunguzwa na upendo[1].

Hata hivyo Visensya aliendeleza shirika lao kwa miaka mingi akafariki mwaka 1847 hukohuko Lovere.

Wote wawili walitangazwa wenye heri na Papa Pius XI tarehe 30 Mei 1926, halafu watakatifu na Papa Pius XII tarehe 18 Mei 1950.

Sikukuu ya Bartolomea inaadhimishwa kila mwaka tarehe 26 Julai[2].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads