Billie Jean
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
"Billie Jean" ni wimbo wa dance-pop R&B wa msanii Michael Jackson. Wimbo huu ulitungwa na Jackson na kutayarishwa na Quincy Jones kwa ajili ya albamu yake ya sita Thriller (1982). Yenyewe haikupendwa na Jones, wimbo huu almanusura itolewe kwenye albamu baada ya yeye na Jackson kuwa na malumbano kadhaa.
Mashairi yaliyomo yanahusu maisha halisi ya binadamu, ambamo inazungumzia mwanamke mmoja mgonjwa wa kichaa anayedai kwamba Jackson amezaa naye watoto pacha.
Wimbo unajulikana sana kwa besi lake na staili ya sauti ya Jackson. Wimbo huu ulimwezesha Michael kuzidi kuwa maarufu hasa pale alipokuwa akiuimba moja kwa moja jukwaani akiutumia mtindo wa kucheza huku akirudi nyuma nyuma kwa kutumia miguu yake pasipo kuanguka. Kwa lugha ya Kiingereza mtindo huu unafahamika kama Moon Walker. Wachezaji wengi wa muziki duniani wanautumia mtindo huu wa dansi katika maonesho mbalimbali ya kimuziki majukwaani.
Remove ads
Chati
Matunukio
Remove ads
Maelezo
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads