Biofueli
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Biofueli ni aina ya nishati inayozalishwa kutoka vyanzo vya kikaboni, kama mimea au viumbe hai vingine, badala ya kutegemea fueli za kisukuku ambayo ni mabaki ya viumbehai ya miaka mingi iliyopita kama mafuta ya petroli au makaa ya mawe. Biofueli hupatikana kama dutu mango, kiowevu au gesi.

Mara nyingi biofueli inatumika kama nishati mbadala ya kuendesha injini za magari na ndege, na hata kwa kuzalisha umeme au kuwasha moto nyumbani. Kwa kuzingatia upatikanaji wa vyanzo vyenye kaboni, biofueli inaonekana kama suluhisho linalopunguza utegemezi wetu kwa vyanzo vya nishati vinavyochangia mabadiliko ya tabianchi[1].
Kuna mbinu mbili hasa za kutengeneza biofueli:
- kulima mimea yenye kiwango kikubwa cha sukari au wanga kama muwa. Kwa msaada wa bakteria wanga au sukari hubadilishwa kuwa alikoholi (ethanoli).
- kulima mimea yenye kiwango kikubwa cha mafuta katika mbegu au miili yao kama algae, michikichi (mawese) au soya.

Ethanoli hizi hutumiwa badala ya petroli na mafuta badala ya diseli katika injini ya mwako ndani.
Njia nyingine ni kutumia mbao au nyasi mbalimbali zilizokaushwa, na mara nyingi kukatwa na kupewa umbo la donge halafu kuchomwa kwa kutengeneza umeme.
Remove ads
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads