Muwa

From Wikipedia, the free encyclopedia

Muwa
Remove ads

Miwa (Saccharum spp.) ni aina za nyasi zinazotoa sukari.

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi ...

Asili yake ilikuwa Asia ya Mashariki na kutoka huko zimesambazwa katika nchi za tropiki zenye mazingira yanayofaa kwake.

Kilimo cha mmea huo ni chanzo cha sehemu kubwa ya sukari kwa ajili ya matumizi ya binadamu na pia kwa sehemu kubwa ya ethanoli inayotengenzwa kwa matumizi ya biofueli.

Kwa ajili yake katika karne za nyuma ilistawi biashara ya watumwa hasa kutoka Afrika kwenda Amerika.

Remove ads

Kilimo

Muwa hulimwa kote katika nchi za kitropiki ukiwa ni chanzo cha asilimia 55 ya mahitaji ya sukari duniani. Nchi zinazolima muwa kwa wingi ni (uzalishaji wa mwaka 2005 kwa tani 1.000)

Nchi za Afrika ya Mashariki huzalisha kiasi kidogo tu duniani kama Tanzania (tani 300,000), Kenya (5,112,000) na Uganda (2,350,000).[1].

Kati ya mwaka 2004 na 2008 uzalishaji duniani uliongezeka kutoka tani bilioni 1.34 kufikia tani bilioni 1.74. [2]

Remove ads

Picha

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads