Blandina Changula
Mwigizaji filamu wakike kutoka Tanzania From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Blandina Changula (alizaliwa mkoani Shinyanga, Tanzania, 28 Julai 1984) ni muigizaji na mtayarishaji wa vipindi vya televisheni na filamu nchini Tanzania.
Remove ads
Maisha ya mwanzo
Blandina alipata elimu ya msingi katika shule ya Bugoyi mwaka 1990 hadi 1997 na kujiunga katika shule ya sekondari ya kutwa ya Buluba iliyopo Shinyanga mwaka 1998 hadi 1999.
Akiwa kidato cha pili alihamishiwa katika shule ya bweni ya Kanawa hukohuko mkoani Shinyanga mwaka 1999 hadi 2000 na mwaka huo huo baada ya kuingia kidato cha tatu akahamishiwa tena jijini Dar es Salaam katika shule ya Greens iliyokuwa maeneo ya Temeke kabla ya kuhamishiwa Ubungo shule ambayo alimalizia kidato cha nne hiyo ilikuwa mnamo mwaka 2001.
Blandina Changula anatokea kundi la Kaole Sanaa Group, ni kundi ambalo linafahamika sana nchini Tanzania kwa kutoa nyota wengi waigizaji, Blandina nae ni mmoja kati ya nyota hao, wengine ni Steven Kanumba, Vincent Kigosi (Mr Ray), Thea na wengine wengi tu kutoka Kaole Sanaa Group.
Blandina Changula kwa kushirikiana na msanii mwenzake Vincent Kigosi (Ray) waliunda kampuni iitwayo RJ Company (Ray & Johari company) ambayo ilifanya kazi ya kuzalisha filamu mbalimbali kama vile Bed Rest, Bad Luck, Wrong Hope, Peace of Mind, Fair Decision.
Kwa sasa Blandina Chagula ni mmliki wa kampuni ya utengenezaji wa filamu iitwayo Empire Lokoma ambayo imetayarisha Tamthilia ya Maji ya shingo.
Remove ads
Baadhi ya filamu alizoigiza
- Sikitiko Langu
- Johari 1 na 2
- Dangerous Desire
- Dar 2 Lagos
- Yellow Banana
- Bad luck
- Mke mchafu
Alioshirikiana nao
- Steven Kanumba
- Vincent Kigosi
- Muhsein Awadh
- Ally Chaowa
- Kulwa Kikumba
- Mwanaidi Suka
- Nuru Nassoro
- Ndumbagwe Misayo
- Donah Redson
- Fatuma Makongoro
- Emmanuel Myamba
- Charles Magari
- Fatuma Mvura
- Mohamed Mwikongi
- Fadhili Omar
Wanigeria
- Mercy Johnson
- Nkilu Sylvanus
- Nancy Okeke
- Bimbo Ankintola
| Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Blandina Changula kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads
