Steven Kanumba

Muigizaji wa filamu, mwandishi na mkurugenzi (1984-2012) From Wikipedia, the free encyclopedia

Steven Kanumba
Remove ads

Steven Charles Kanumba (mkoa wa Shinyanga, 8 Januari 1984 [1]katika - 7 Aprili 2012 [2]) alikuwa msanii wa maigizo na filamu kutoka Tanzania. Ni mmoja wa wasanii wa kwanza kufanya kazi nje ya nchi na kuvutia wasanii wa nje kuja kuigiza nchini Tanzania, hasa Wanigeria kama vile Mercy Johnson, Emmanuel France, Nkiru Silvanus, Ramsey Nouah [3]. Kanumba pia ameweza kuwaleta waongozaji filamu kadhaa wa Kinigeria nchini.

Ukweli wa haraka Amezaliwa, Amekufa ...
Remove ads

Maisha

Baba yake alikuwa anaitwa Charles Kanumba na mama yake aliitwa Flora Mutegoa. Alikuwa ana uwezo wa kuongea lugha 3: Kiswahili, Kisukuma na Kiingereza.

Steven alianza elimu yake ya msingi katika Shule ya msingi Bugoyi na aliendelea na elimu ya sekondari katika Shule ya Sekondari Mwadui. Baadae alihamishiwa Vosa Mission Secondary School. Alijiunga na kidato cha 5 & 6 katika Shule ya Sekondari Jitegemee[4] iliyopo Dar-es-Salaam

Remove ads

Shughuli za uigizaji

Kanumba ameanza shughuli za kuigiza miaka mingi kwenye miaka ya 1990. Ambapo alianza kufahamika zaidi mwaka 2002 mara tu baada ya kujiunga na kundi la sanaa ya maigizo maarufu kama Kaole Sanaa Group lililopo Bagamoyo. Alijibebea umaarufu mkubwa nchini Tanzania na alikuwa kipenzi cha wengi na alikubalika karibia nchi zote za Afrika Mashariki na maziwa makuu. Aliweza kutangaza sanaa nchi za Afrika ya Magharibi ikiwemo Nigeria na pia Wanigeria walipendezewa na uigizaji wake hivyo kushirikiana pamoja naye katika filamu kadha wa kadha. Filamu ambazo aliwahi kuigiza ni Dar to Lagospamoja na She is My Sister .

Remove ads

Kifo

Kanumba alifariki baada ya kupata jeraha kwenye ubungo, ambapo jeraha hilo lilisabishwa baada ya kupata pigo kichwani tarehe 07/04/ 2012 [5] ILisemekana alikuwa na rafiki yake wa kike anayeitwa Elizabeth Michael anaye fahamika kama Lulu ambaye alikuwa na miaka 18 kipindi hicho. Lakini rafiki yake huyo alikanusha kuhusu kuhusika na kifo cha Kanumba.[6] Kanumba alipelekwa hospitali ya taifa Muhimbili akiwa mahututi ambapo, baada ya vipimo madktari walithibitisha kwamba kifo chake kilitokana na jeraha kwenye ubungo kumsababishia kukosa pumzi na kupoteza uhai hapo. Mnamo mwaka 2017, Lulu alituhumiwa kwa kuua bila kukusudia na alipewa adhabu ya kufungwa miaka 2.[7] Hukumu yake ilibadilishwa na kufanya huduma za kijamii aliachiwa jela baada ya kifungo cha mwaka mmoja released from jail 12/05 /2018. Msiba wake ulihudhuriwa na watu takribani 30,000 akiwepo mheshimiwa mama Salma Kikwete. Alizikwa katika makaburi ya Kinondoni.

Filmografia

Televisheni

  • Jahazi
  • Dira
  • Zizimo
  • Tufani
  • Sayari
  • Taswira
  • Gharika
  • Baragumu

Filamu

Maelezo zaidi Mwaka, Jina ...
Remove ads

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads