Ubungo

From Wikipedia, the free encyclopedia

Ubungo
Remove ads

(makala hii inahusu kata ya Ubungo, kuangalia makala ya wilaya yake bonyeza hapa)

Ukweli wa haraka Nchi, Mkoa ...
Thumb
Mtazamo wa angani wa Wilaya ya Ubungo unaoangalia makao makuu ya kampuni ya umeme ya TANESCO kushoto.

Ubungo ni kata ya wilaya ya Ubungo katika Mkoa wa Dar es Salaam, Tanzania, yenye postikodi namba 16103.

Ubungo ipo katika sehemu ya kati ya magharibi mwa wilaya na inafahamika sana Tanzania kama kitovu kikuu cha Mabasi yaelekeayo mikoani.

Kituo cha mabasi cha Ubungo kimeungana na baadhi ya vituo vikubwa vya miji mbalimbali ya Tanzania kama vile cha Arusha, Moshi, Morogoro, Dodoma, Mbeya, Iringa, Mtwara, Lindi, Singida, Tanga na Mwanza; vilevile hadi Nairobi, Lilongwe, Lusaka na miji mingine kadhaa ya Afrika ya Mashariki.

Pia Ubungo ndipo palipo makao makuu ya TANESCO, shirika la umeme la Tanzania.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 44,340 [1].

Remove ads

Tanbihi

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads