Boroni
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Boroni ni elementi ya kikemia yenye namba atomia 5 kwenye mfumo radidia na uzani atomia 10.811. Alama yake ni B.
Remove ads
Tabia
Boroni ni nusumetali au metaloidi; ina valensi tatu. Elementi peke yake haipatikani katika mazingira asilia duniani ila tu katika kampaundi kama vile borasi (Na2B4O7·10H2O ).
Umbo hobela au la fuwele
Inapotapaswa kutoka kwa kampaundi zake hupatikana katika umbo hobela kama unga wa rangi ya kahawia au la fuwele nyeusi na ngumu isiyohami umeme. Boroni ni dutu ngumu kuliko zote duniani baada ya almasi na kati ya elementi zote ni imara dhidi ya nguvu ya mvuto.
Matumizi kiteknolojia
Matumizi ya boroni ni katika teknolojia ya kihami na katika dawa za kupausha au kung'arisha. Inatumiwa pia kama nyongeza katika aloi kwa ajili ya sehemu za eropleni zinazotakiwa imara ma nyepesi. Katika teknolojia ya kinyuklia hutumiwa kama kinga dhidi ya nyutroni katika matanuri ya nyuklia.
Nafasi ya kibiolojia
Kwa kiasi kidogokidogo boroni ina kazi katika miili ya wanyama: haijaeleweka ni kazi gani, isipokuwa imeonekana ni muhimu. Asidi ya boroni ni kiuawadudu (insecticide), hasa dhidi ya sisimizi, viroboto na mende, lakini haiudhi wanyama wenye uti wa mgongo.[1]
Picha
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads