Mbwa-mwitu Dhahabu

From Wikipedia, the free encyclopedia

Mbwa-mwitu Dhahabu
Remove ads

Mbwa-mwitu dhahabu (pia bweha-dhahabu, bwea dhahabu, mbweha dhahabu na bweha-mbuga) ni mnyama wa jamii ya mbwa anayetokea Afrika ya Kaskazini na ya Mashariki. Zamani jina lake la kisayansi lilikuwa Canis aureus, lakini hivi karibuni wataalamu wamebaini kwamba nususpishi za Afrika ni tofauti na zile za Asia na Ulaya. Kwa hivyo nususpishi za Afrika zimepata jina jipya Canis anthus[1]. Hadi sasa bado huitwa bweha na watu wengi lakini yuko karibu zaidi na Mbwa-mwitu Habeshi na Mbwa-nyika (coyote) wa Amerika ya Kaskazini. Kwa hivyo tafadhali aitwe mbwa-mwitu.

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...

Anapatikana Kenya na kaskazini kwa Tanzania (k.m. Hifadhi ya Serengeti) ambayo ni kusini kabisa ya uenezaji wake.

Mbwa-mwitu dhahabu hula wanyama wadogo hadi ukubwa wa swala, mizoga, wadudu na matunda. Makazi yake ni jangwa, mbuga na misitu myepesi. Anaishi kwa vikundi vidogo hasa dume na jike pamoja na watoto.

Kwa jumla kuna nususpishi 6 zinazo tambuliwa:

Remove ads

Tanbihi

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads