Salamanda

From Wikipedia, the free encyclopedia

Salamanda
Remove ads
Remove ads

Salamanda ni wanyama wa oda Caudata katika ngeli Amfibia wafananao na mijusi. Wanatofautiana na vyura kwa kuwa na mkia hata katika hatua ya mnyama mzima. Ngozi yao haina magamba na ni laini na nyevu, lakini ngozi ya spishi nyingi za familia Salamandridae ni kama mahameli au ina sugu. Rangi ya salamanda ni nyeusi, kijivu au kahawia kwa kawaida, lakini madume ya spishi nyingi hupata rangi kali wakati wa kuzaa. Spishi kadhaa zina sumu katika ngozi yao na hizi zina daima madoa au milia ya rangi kali ili kuonya wanyama mbuai. Takriban salamanda wote wanatokea nusudunia ya kaskazini, lakini spishi kadhaa zinatokea Amerika ya Kusini. Spishi nne zinatokea Afrika tu, huko kaskazini (Maroko, Aljeria na Tunisia).

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Remove ads

Ndubwi

Ndubwi au viluwiluwi wa salamanda wanafanana na hawa wa vyura lakini wale wa salamada ni wembamba zaidi na matamvua yao ni makubwa kwa kawaida kuliko yale ya ndubwi wa vyura. Kabla ya kutoka maji wanakuza miguu minne. Spishi nyingi za Plethodontidae (salamanda bila mapafu) hazina ndubwi lakini mayai hutagwa nchini kavu na salamanda wadogo, siyo ndubwi, hutoka.

Spishi za Afrika

Picha

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads