Chelsea F.C.
kilabu ya mpira huko London, Uingereza From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Chelsea Football Club[5][6] [7][8]ni klabu ya mpira wa miguu ya nchini Uingereza iliyo na maskani yake Fulham, London. Klabu hii ilianzishwa mwaka 1905, na kwa miaka mingi sana imekuwa ikishiriki ligi kuu ya Uingereza. Uwanja wao wa nyumbani ni Stamford Bridge ambao una uwezo wa kuingiza watazamaji 41,837, wameutumia uwanja huu tangu klabu ilivyoanzishwa.
Chelsea, kwa mara ya kwanza ilipata mafanikio makubwa mwaka 1955, ambapo walipata ubingwa wa ligi, na walishinda mataji kadhaa katika miaka ya 1960, 1970, 1990 na 2000. Klabu hii imefurahia zaidi mafanikio katika miongo miwili ilopita, kwa kushinda mataji makubwa 15 tangu mwaka 1997.
Nyumbani, Chelsea imeshinda ubingwa wa ligi mara nne, kombe la FA mara saba, kombe la ligi mara nne, pamoja na ngao za jamii mara nne. Na kimataifa Chelsea imeshashinda UEFA Cup Winners' Cups mara mbili, UEFA Super Cup moja, UEFA Europa League mara mbili na UEFA Champions League mara mbili. Chelsea ndio klabu pekee kutoka London kushinda UEFA Champions League, na ni moja kati ya klabu nne kutoka Uingereza, kuchukua makombe yote makubwa matatu ya Ulaya.
Kwa kawaida Chelsea huvaa jezi ya bluu, kaptula ya bluu na soksi nyeupe. Nembo ya klabu imebadilishwa mara nyingi kulingana na wakati na kuboresha muonekano wa klabu. Nembo ya sasa inaonesha picha ya simba akiwa amebeba mkuki. Tangu Julai 2003, Chelsea imekuwa ikimilikiwa na bilionea wa Kirusi, Roman Abramovich. Tarehe 7 Mei 2022, Chelsea ilithibitisha kwamba masharti yametimiza na kikundi kipya cha umiliki, kinachoongozwa na Todd Boehly, Clearlake Capital, Mark Walter na Hansjörg Wyss, kununua klabu hiyo.[9] Mnamo tarehe 25 Mei 2022, serikali ya uingereza iliidhinisha kuuzwa kwa Chelsea kwa £4.25bn. Mnamo tarehe 30 Mei 2022, mauzo yalikamilika, na hivyo kumaliza umiliki wa miaka 19 wa Abramovich.[10]
Remove ads
Wachezaji
Kikosi cha timu ya kwanza
Kama ilivyokuwa tarehe 10 Agosti 2022, kulingana na vyanzo mseto katika tovuti rasmi.[11]
- As of 31 August 2024[12]
Note: Flags indicate national team as has been defined under FIFA eligibility rules. Players may hold more than one non-FIFA nationality.
Nje kwa mkopo
- As of 31 August 2024[13]
Note: Flags indicate national team as has been defined under FIFA eligibility rules. Players may hold more than one non-FIFA nationality.
Mchezaji Bora wa Mwaka
Chanzo: Chelsea F.C.
Remove ads
Tuzo
- Ligi Kuu (6) 1954-1955, 2004-2005, 2005-2006, 2009-2010, 2011-2012, 2016-2017
- FA Cup (7) 1970, 1997, 2000, 2007, 2009, 2010, 2018
- Kombe la Ligi (4) 1965, 1998, 2005, 2007;
- Ngao ya Jamii (4) 1955, 2000,2005, 2009
- UEFA Cup Winners' Cup (2) 1971, 1998
- UEFA Super Cup (1) 1998, 1999, 2003
- Ligi ya Mabingwa Ulaya (2) 2012, 2021
- Kombe la Ulaya (2) 2013, 2020
- Full Members Cup (2) 1986, 1990
- FA Youth-cup (3) 1960, 1961, 2010
Remove ads
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads