Ufini
nchi katika Ulaya Kaskazini From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Ufini , (kwa Kifini: Suomi) rasmi kama Jamhuri ya Ufini ni nchi ya Skandinavia iliyoko Ulaya ya Kaskazini. Imepakana na Norwei upande wa kaskazini, Urusi upande wa mashariki na Uswidi upande wa magharibi. Ng'ambo ya Baltiki iko Estonia ambayo watu wake hutumia lugha iliyo karibu sana na Kifini. Inaonekana ya kwamba mababu wa Wafini na Waestonia walihama pamoja wakiwa na lugha ileile zamani, lakini sasa ni lugha mbili kwa sababu hawakuwa na mawasiliano kati yao kwa muda mrefu.

Ufini ina idadi ya watu takriban milioni 5.6 na mji mkuu wake ni Helsinki, ambao pia ni mji mkubwa zaidi nchini. Nchi hii ina mazingira ya kuvutia yenye maziwa mengi (takriban 188,000) na misitu mikubwa inayochukua sehemu kubwa ya ardhi yake. Ufini pia hujulikana kwa kuwa na majira ya baridi kali na mchana mfupi wakati wa majira ya baridi kaskazini, huku maeneo ya Aktiki yakipata kipindi cha usiku mrefu wa majira ya baridi na mwanga wa saa 24 wakati wa majira ya joto.
Kiutawala, Ufini ni jamhuri ya kidemokrasia yenye mfumo wa serikali ya bunge. Rais ni mkuu wa nchi, wakati waziri mkuu ndiye mkuu wa serikali. Ufini ni mwanachama wa Umoja wa Ulaya, Umoja wa Mataifa, Baraza la Nordic, na kuanzia 2023, mwanachama wa NATO. Nchi imepata sifa duniani kwa viwango vyake vya juu vya elimu, haki za binadamu, usawa wa kijamii, na ustawi wa wananchi. Ufini pia huchukuliwa kuwa moja ya nchi zenye viwango vya juu vya furaha duniani.
Remove ads
Historia
Historia ya awali
Ufini ulikaliwa na watu tangu ilipokwisha enzi ya barafu ya mwisho, miaka 9000 KK hivi.[4] Wakazi wa kwanza walikuwa wawindaji-wakusanyaji ambao walitumia vifaa vya mawe vinavyofanana na vile vya Estonia, Russia na Norway.
Karne za kati
Mwishoni mwa karne ya 13 Ufini ukawa sehemu ya Sweden hadi mwaka 1809, ilipomezwa na Urusi kama ufalme mdogo wenye kujitawala kwa kiasi fulani.
Karne ya 20

Mwaka 1906, Ufini ulikuwa nchi ya kwanza duniani kuwapa wananchi wote wenye umri wa utu uzima haki ya kugombea vyeo vya serikali.[6][7]
Mwaka 1917, baada ya Mapinduzi ya Russia, Ufini ulijitangaza huru na mwaka uliofuata ukawa jamhuri baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Wakati wa vita vikuu vya pili, Muungano wa Kisovyeti ulijitahidi kuteka Ufini wote, ukaishia kutwaa Karelia, Salla, Kuusamo, Petsamo na visiwa kadhaa tu.
Baada ya vita Ufini uliacha kutegemea kilimo ukajitosa katika uchumi wa viwanda[8] hata kufikia kuwa kati ya nchi zilizoendelea zaidi[9][10][11][12][13][14][15].
Mwaka 1955 Ufini ulijiunga na Umoja wa Mataifa ukichagua siasa ya kutoambatana na upande wowote.
Mwaka 1995 ulijiunga na Umoja wa Ulaya na mwaka 1999 ulikubali kutumia euro.
Remove ads
Demografia

Kuna jumuiya tatu katika Ufini:
- Wafini wenyewe ambao ni 90% ya wakazi wote.
- Waswidi wako hasa upande wa kusini mwa nchi, kwa jumla ni takriban 5% ya wakazi; hasa visiwa vya Aland kuna Waswidi watupu walio na hali ya kujitawala ndani ya Ufini.
- Wakazi asilia ni Wasami ambao wako kaskazini tu. Maisha yao yanategemea uwindaji na ufugaji; wako wachache, jumla yao haifikii 0.2% ya wakazi wote.
Mbali na hao, kuna wahamiaji (5.9%), hasa kutoka Russia, Estonia na Somalia.
Lugha rasmi ni Kifini na Kiswidi. Lugha ya Kifini ina asili ya Asia ya Kati, haina uhusiano na lugha za Kihindi-Kiulaya.
Wakazi wenye lugha ya Kiswidi wako upande wa kusini mwa nchi kwa sababu Ufini ilitawaliwa na Uswidi kwa karne nyingi. Katika karne hizo walikuwepo Waswidi waliohamia Ufini lakini kuna pia Wafini walioanza kutumia Kiswidi pekee. Hasa kwenye visiwa vya Aland Kiswidi ni lugha pekee. Lakini Waswidi wa Ufini wanajisikia wa Ufini.
Dini
Upande wa dini, 72% ni Walutheri na 1.1% Waorthodoksi. Madhehebu hayo mawili ya Ukristo yanatambulika na kupewa nafasi katika matukio mbalimbali na shuleni. 1,6% wanafuata dini au madhehebu mengine, wakati 25.3% hawana dini yoyote.
Watu maarufu
- Mikael Agricola
- Urho Kaleva Kekkonen
- Elias Lönrrot
- Garlf Gustaf Emil Mannerheim
- Martti Ahtisaari
- Alvar Aalto
- Jean Sibelius
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads