Chitungwiza

From Wikipedia, the free encyclopedia

Chitungwiza
Remove ads

Chitungwiza ni mji wa Zimbabwe, kilometa 9 upande wa kusini wa mji mkuu Harare. Mwaka 2022 ulikuwa na wakazi 371,000[1]. Walio wengi wanafanya kazi Harare kwa sababu kuna nafasi chache tu za ajira.

Thumb
Kituo cha manunuzi Chitungwiza.

Chitungwiza ilipata hadhi ya manispaa mwaka 1981 na ni wilaya mojawapo kati ya tatu za mkoa wa Harare. Asili yake ni mitaa mitatu ya Seke, Zengeza na St Marys iliyojengwa wakati wa ubaguzi wa rangi kama makazi ya Waafrika wasioruhusiwa kukaa Harare penyewe.

Siku hizi Chitungizwa ni mji wa kukua haraka Zimbabwe. Kiwanja cha ndege cha Harare kipo karibu.

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads