Rasi ya Chukchi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Rasi ya Chukchi (pia Rasi ya Chukotka; kwa Kirusi: Чуко́тский полуо́стров, Chukotskiy poluostrov au Чуко́тка Chukotka) ni rasi ya mashariki zaidi ya Asia. Upande wa mashariki inaishia kwenye Rasi Dezhnev karibu na kijiji cha Uelen.



Imepakana na Bahari ya Chukchi upande wa kaskazini, Bahari ya Bering upande wa kusini, na Mlango wa Bering upande wa mashariki. Rasi hii ni sehemu ya Okrug huru ya Chukotka ya Urusi [1]. Wakazi wake ni makabila ya watu asilia wa Siberia na walowezi wachache Warusi.
Tasnia kwenye rasi hiyo ni pamoja na madini (bati, risasi, zinki, dhahabu, na makaa ya mawe) uwindaji, ufugaji wa kulungu aktiki, na uvuvi.
Remove ads
Marejeo
Kusoma zaidi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads